SEKTA YA USAGISHAJI MAHINDI TANZANIA: FURSA & CHANGAMOTO ZAKE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SEKTA YA USAGISHAJI MAHINDI TANZANIA: FURSA & CHANGAMOTO ZAKE

Mashine ya kusaga sembe na dona

SEMINA SIKU YA KWANZA

SEKTA YA USAGISHAJI NAFAKA (MAHINDI)

Unga wa mahindi hutumika na karibu kila Mtanzania kutengeneza chakula maarufu kiitwacho ugali. Kulinagana na taarifa za Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) zao la mahindi huchukua zaidi ya asilimia 74.3% ya uzalishaji wa nafaka zote nchini Tanzania na asilimia 66% ya mazao yote yanayolimwa nchini kwa mwaka.

Sekta ya usagishaji nafaka hususani mahindi nchini Tanzania imeshuhudia mabadiliko makubwa tangu kufunguliwa kwa soko huria miaka ya 90s ambapo lililokuwa Shirika la Usagishaji la Taifa NMC lilibinafsishwa kwa wafanyabiashara wakubwa na makampuni binafsi. Sekta ina wasagishaji wakubwa waliotapakaa zaidi mijini  na wasagishaji wadogowadogo waliojikita zaidi maeneo ya vijijini.

Kwa mujibu wa Shirika la SIDO tafiti zinaonyesha kuwa wasagishaji wadogo wengi hawakidhi vigezo vya usafi na usalama vilivyowekwa na SIDO pamoja na OSHA huku pia wakikabiliwa na tatizo la ukosefu wa mikopo ya kupanua biashara zao.

Washiriki kwenye sekta hii

Kuna takriban makampuni makubwa manne kwenye sekta yanayomiliki maghala na miundombinu mikubwa ya usagishaji nafaka ambayo ni; Salim Salim Bakhresa (SSB), Mohamed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL) na Export Trading Group (ETG) na Azania Group. Lakini pia hivi karibuni Serikali ilifufua upya lililokuwa Shirika la usagishaji la Taifa NMC lakini safari hii likijulikana kama Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko (CPB)  

Pamoja na Makampuni hayo makubwa 5 kuna makampuni mengine mengi madogomadogo yanayoibuka kila siku kutokana na fursa kubwa iliyopo kwa sekta hii. Makampuni madogo ya usagishaji mahindi yapo mijini lakini pia vijijini.

Usafirishaji kwenye sekta

Makampuni makubwa na ya kati yamewekeza katika miundombinu ya usafirishaji nafaka karibu kila kona ya nchi ili kuwafikia wauzaji wa jumla na rejareja wakati kampuni ndogondogo zinazosagisha mahindi wastani wa chini ya tani moja kwa siku, wao hutegemea zaidi kusambaza bidhaa zao za unga katika maeneo walipo hasa kwa wenye maduka ya jumla na rejareja mitaani na kwenye masoko yaliyo karibu.  

Changamoto kubwa kwenye sekta

Baadhi ya changamoto zinazowakumba wasagishaji mahindi hasahasa wale wadogo wanaosaga mpaka tani 1 kwa siku ni pamoja na;

1.   Ubora hafifu wa mahindi yanayozalishwa na wakulima wadogowadogo kwani utakuta mahindi mengi yamejaa vumbi na hayatoi uwiano mzuri wa unga (kande) na pumba

2.   Upatikanaji usiokuwa wa uhakika wa mahindi unaosababisha wasagishaji wadogo wenye mitaji kidogo kushindwa kukabiliana na ongezeko la bei ya mahindi pindi yanapoadimika.

3.   Ukosefu wa mikakati madhubuti ya uuzaji wa mahindi ndani na nje ya nchi, kwa mfano sasa hivi sekta inashuhudia ongezeko kubwa la wafanyabisahara kutoka nchi jirani  kuja na kununua mazao ya mahindi mpaka pumba na kusababisha bidhaa hizo kuadimika au bei kupanda mara mbili.

Hii inaweza ikawa fursa kwa wafanyabiashara na wakulima lakini inafaa kuwe na udhibiti hasa katika bei mahindi yasijekununuliwa kwa bei ya chini mno kuliko ilivyopasa kuwa.

Fursa zilizokuwepo              

Pamoja na changamoto zilizotajwa pale juu, biashara ya usagishaji wa mahindi bado imejaa fursa nyingi kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kwani mahindi yanabakia kuwa ndio zao kuu la chakula kwa karibu watu wote wa ukanda huu wa Afrika ya Mashariki, Kati na Kusini.

Ongezeko kubwa la watu, ukame na hali mbaya ya hewa vinafanya mahitaji ya mahindi kuwa makubwa zaidi hivyo kuongezeka fursa kwenye sekta.

Kwa mfano ukiangalia mwaka huu wa 2024 maeneo mengi nchini Tanzania hayakuwa na mvua za kutosha za vuli hivyo wasagishaji walio na mitaji mikubwa wanaweza badala ya kuuza kwa bei ya chini bidhaa zao nje ya nchi wakayahifadhi mahindi na kusubiri kipindi bei ya mahindi itakapokuwa juu wakaja kusaga na kuuza kwa faida zaidi.

Umuhimu na Faida za semina hii

Leo tumeanza rasmi semina kubwa ya kufunga mwaka ya siku 7. Semina hii ni kwa ajili ya mtu anayependa kujifunza jinsi ya kuandika mchanganuo wa biashara yeyote ile. 

Tumetumia mchanganuo maalumu wa biashara ya usagishaji nafaka (Dona & Sembe) kama kielelezo lakini masomo 11 ya awali katika semina hii yanalenga mtu kujifunza kwa ujumla namna ya kuandika mchanganuo wa biashara yeyote ile.

Hapa tumeanza na kuielezea sekta ya usagishaji mahindi ilivyo nchini Tanzania ili kutoa picha halisi ya sekta nzima kwa ujumla kisha masomo yenyewe ya semina yanaendelea. 

Unapojiunga na semina hii unaanza darasa siku hiyohiyo kwani tuna madarasa asubuhi, mchana na jioni kila siku hadi mwisho wa OFFA hii. 

Siku 7 zinaanza pale tu unapojiunga na utapangiwa darasa na wenzako walioanza siku hiyohiyo au siku moja kabla ili kwenda pamoja kisha mwishoni wanafunzi wote hukutana MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO kwa ajili ya mentorship kila siku na masomo mengine ya fedha, mijadala na kutanganza bidhaa & huduma zao wanazotoa  kwa mwaka mzima bure

Mfanyabiashara yeyote awe mkubwa au mdogo anahitaji kufahamu 'ABC' za mchanganuo wa biashara haijalishi anataka kuandika ama la, ipo siku utahitaji hata kuandikiwa na mtaalamu mchanganuo wako sasa ikiwa hujui hata ABC moja unadhani atakayekuandikia akikuongopea mahali utajuaje?

Kozi hii pia inamfaa mtu yeyote anayetaka kubobea kwenye uandishi wa michanganuo ya biashara kama mimi. Kuandika Michanganuo ya watu wengine ni biashara isiyopitwa na muda 'as long as' biashara itadumu miaka yote binadamu ataishi kwenye hii sayari ya Dunia

 

 

RATIBA YA SEMINA

 

SIKU YA KWANZA: 

·      Utangulizi – Sekta ya Usagishaji nafaka Tanzania

·      Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mchanganuo wa biashara yeyote ile

SIKU YA PILI:

MCHANGANUO WA BIASARA YA USAGISHAJI UNGA WA SEMBE NA DONA HATUA KWA HATUA

·      Muhtasari

·      Maelezo ya Biashara

SIKU YA TATU:

MCHANGANUO WA BIASARA YA USAGISHAJI UNGA WA SEMBE NA DONA HATUA KWA HATUA

·      Maelezo/Tathmini ya Soko

 

        SIKU YA NNE:

MCHANGANUO WA BIASARA YA USAGISHAJI UNGA WA SEMBE NA DONA HATUA KWA HATUA

·      Mikakati & Utekelezaji

 

        SIKU YA TANO:

MCHANGANUO WA BIASARA YA USAGISHAJI UNGA WA SEMBE NA DONA HATUA KWA HATUA

·      Uendeshaji

·      Uongozi & Wafanyakazi

 

SIKU YA SITA:

MCHANGANUO WA BIASARA YA USAGISHAJI UNGA WA SEMBE NA DONA HATUA KWA HATUA

·      Mpango wa Fedha sehemu ya 1

 

SIKU YA SABA:

MCHANGANUO WA BIASARA YA USAGISHAJI UNGA WA SEMBE NA DONA HATUA KWA HATUA

·      Mpango wa Fedha sehemu ya 2

·      Viambatanisho muhimu

 

Karibu sana ushiriki nasi kwa kulipa ada yako sh. 10,000/= Baada ya malipo, kwanza unatumiwa  papo hapo OFFA ya vitabu na michanganuo jumla vitu 12 kwenye simu au kompyuta yako, kisha nakuunganisha Mastermind Group la Michanganuo-online2025 kwa mwaka mzima kwa ajili ya masomo ya fedha, mijadala na kozi za michanganuo mifupimifupi ya biashara zenye ubunifu mkubwa

Kumbuka mwaka 2025 tumeandaa programu bunifu kabambe ambayo itahusisha moja kwa moja vitendo halisi na si nadharia tena, tuna mashamba darasa tayari kwa ajili ya kufundishia michanganuo ya biashara zinazolipa haraka kwa vijana na mtu yeyote 'anayestruggle' (kuhangaika) kupata mtaji wa kutosha kwa ajili ya kutoka kibiashara. 

Biashara hizo za mitaji midogo zimefanyiwa majaribio na tutakuwa tukizionyesha 'live' huku washiriki nao wakifuatisha kuzifanya na kuona matokeo yake moja kwa moja.  

Ikiwa hutapata fursa ya kushiriki semina hii unaweza kufuatilia dondoo mbalimbali hapa katika blogu yako hii ya jifunzeujasiriamali ingawa tumeweka tu baadhi ya mambo na siyo semina nzima.

OFFA hii ya vitu 12 ni ya mwisho kwa mwaka huu na umebakia muda mchache sana kumalizika rasmi. Hatutakuwa tena na semina kama hii mwakani 2025. Hii ni fursa pekee ya kujifunza jinsi ya kuandaa mchanganuo wa biashara yeyote ile kwa gharama nafuu kabisa kuwahi kutokea kisha unaendelea kuwa kwenye Darasa la uangalizi (mentorship class) kwa mwaka mzima 

Kumbuka pia faida kubwa ya kujua kuandaa mchanganuo wa biashara ni sawa na kujifunza somo la Biashara kwa ujumla wake kwani unafahamu kila kipengele kinachohusiana na biashara kuanzia mtaji, bidhaa, masoko, usimamizi, mikakati na fedha.


OFFA INAYOMALIZIKA 2024 HII NI HAPA;

                           1.      KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali

                           2.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa

                           3.      KITABU: Toleo jipya la Elimu ya  pesa na Mafanikio

                           4.      KITABU: Sayansi & Sanaa ya Upishi wa chapatti laini.

                           5.      MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji unga wa Dona (USADO Milling)

                           6.      MCHANGANUO: Ufugaji kuku wa nyama (Tumaini Broilers)-Kiswahili &kiingereza

                           7.      MCHANGANUO: Ufugaji kuku chotara Kuroiler-nyama

                           8.      MCHANGANUO: Kilimo cha tikiti maji (Kibada watermelon)

                           9.      MCHANGANUO: Uboreshaji Mashamba ya zabibu Dodoma (Makupila Real Estate)

                        10.    MCHANGANUO: Biashara ya kuuza chipsi

                        11.    MCHANGANUO: Biashara ya mgahawa (Jane Restaurant) Kiswahili & Kiingereza

                        12.    KITABU: Jinsi ya kuandika mchanganuo mfupi wa biashara

 

   JINSI YA KUFANYA MALIPO

Namba za malipo ni; 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo, kisha tuma ujumbe wa sms au watsap usemao “NATAKA OFFA YA MWISHO YA 2024 PAMOJA NA GROUP LA MENTORSHIP 2025” Mara moja nitakutumia zawadi zako zote 12 pamoja na kukuunganisha na MASTERMIND-GROUP LA MICHANGANUO la mwaka 2025

AU

Unaweza kuingia kwenye Duka letu hili la vitabu mtandaoni, Selar.co, na kulipia moja kwa moja sh. elfu 10 pasipo hata kuwasiliana na sisi ukitumia mtandao wowote unaotumia halafu utapewa kifurushi cha ZIP utakachodownload zawadi. Unzip kifurushi na kutoa zawadi zako zote 12. Kisha nitakuunga kwenye MASTERMIND GROUP muda huohuo 

NB: Ikiwa utalipia kupitia duka hili la mtandaoni unaweza kunikumbusha kwa meseji nikuunganishe endapo nitachelewa kucheki mfumo



SOMA NA HIZI HAPA;

1.     Semina ya kuandika mchanganuo wa biashara ya kiwanda cha tofali za sementi - bado siku 4 tu

2.     Semina: mchanganuo wa kuomba mkopo biashara ya ufugaji wa kuku wa nyama 2000

3.     Biashara 7 nzuri mwaka huu: chagua 1 uingize faida na kipato cha ziada kwa urahisi

4.     Biashara ya mtaji mdogo yenye faida kubwa zaidi tanzania ilivyoshangaza darasa la michanganuo ya biashara

5.     Semina: mchanganuo wa biashara ya kusaga na kuuza unga safi wa dona (usado milling)-1



0 Response to "SEKTA YA USAGISHAJI MAHINDI TANZANIA: FURSA & CHANGAMOTO ZAKE"

Post a Comment