JIRUDISHIE UKUU WAKO TENA (MAKE YOURSELF GREAT AGAIN) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JIRUDISHIE UKUU WAKO TENA (MAKE YOURSELF GREAT AGAIN)

Familia ya Rais Donald Trump

Habari za muda huu mpendwa msomaji wa blogu hii na karibu sana kwenye kampeni ya kufanya mabadiliko makubwa kimaisha 2025. Mwaka hauna rangi na kinachobadilika ni tarehe tu kwahiyo ikiwa kama wewe ni mtu unayependa mwaka huu uwe tofauti na miaka mingine yote naomba usome makala hii yote hadi mwisho. Lakini ikiwa hupendi mabadiliko yeyote yale basi achana nayo usipoteze muda wako wa thamani bure. 

Karibu Sana!

Bila shaka katika maisha yako tangu ulipokuwa mtoto mdogo uliwahi kuwa na ndoto kuwa utakapofikisha umri wa utu uzima utafanya hiki na kile au utamiliki kitu fulani. Ulijiwekea malengo makubwa na pengine mpaka hivi leo haujaweza kuyatimiza yote kama ulivyojiwekea.

Wapo walioota kuja kumiliki majumba makubwa, kuwa na kazi nzuri, kuendesha ndege, kuwa kiongozi wa ngazi ya juu serikalini au siasa, kuwa na mke mzuri, familia nk.

Siyo hivyo tu, katika maisha hayo ya utotoni au hata ujanani inawezekana ulikuwa na vipaji mbalimbali, uwezo katika masomo, uwezo katika nyanja fulani na hata inawezekana sasa hivi wewe ni mzee au mtu wa makamo na katika nyakati fulani za maisha yako uliwahi “kutesa” kwa maana nyingine uliwahi kuwa na maisha mazuri iwe ni katika kipato, masomo darasani, afya au hata mafanikio mengineyo yeyote yale kimaisha ambapo kwa sasa hivi, furaha, amani na mafanikio yote hayo vimetoweka mithili ya donge la barafu.

Wakati ulipokuwa katika nyakati hizo nzuri (Ukiwa katika kilele cha UBORA WAKO), kwa lugha nyingine “ulipokuwa katika good times watu wengine walikuwa wakikuheshimu na hata wewe mwenyewe jambo ulilokuwa ukilisema mbele ya jamii iliyokuwa ikikuzunguka lilikuwa likiheshimika na kufanyiwa kazi mara moja hata ikiwa watu waliokuwepo kwa muda huo walikuwa wamekuzidi umri. Kwa kweli kilikuwa ni kipindi cha furaha kubwa isiyokuwa na kifani kwako.

Kumbuka wakati huo ninaouzungumzia mimi siyo lazima iwe ni wakati ulikuwa umeshakuwa mtu mzima la hasha, kilele cha ubora wako kinaweza hata kikawa ni kipindi ulipokuwa ukisoma shule ya msingi, ukiwa mtoto, ukiwa chuoni, ukiwa kazini nk.Kwa mfano mimi binafsi kipindi cha ubora wangu nakumbuka kilikuwa ni wakati nilipokuwa nasoma shule ya msingi.

Kuna mambo mengi mazuri nayakumbuka niliyokuwa nayafanya wakati huo na moja lilikuwa ni Ucha Mungu uliokuwa umekamilika, nilikuwa na uwezo wa kuombea jambo na kweli nikaona matokeo yake, pia ni kipindi ambacho karibu kila jambo nililolifanya lilifanikiwa kuanzia darasani mpaka shughuli zangu za ufugaji wa kuku na kilimo cha bustani ya mbogamboga na matunda nyumbani.

Sasa hivi ukiwa unajiuliza ni nini hapo katikati kilichokuja kutokea mpaka mambo yakaenda mrama ukapoteza ule ukuu wako uliokuwa nao, nadhani utakuwa na sababu nyingi sana, nyingine ukijilaumu kwa kuzisababisha wewe mwenyewe na nyingi ukitoa lawama kwa watu mbalimbali na hata serikali kwamba bila ya wao leo hii usingelikuwa umepoteza ukuu uliokuwa nao.

Lakini lawama kwako au hata kwa watu wengine na serikali haziwezi zikabadilisha kitu chochote kile kwani hatima ya maisha yako ipo mikononi mwako mwenyewe na ni wewe unayeweza kuamua kuibadilisha au kufanya iendelee kuwa vilevile kama ilivyo leo.

Mwaka huu mpya wa 2025, nimeandaa kampeni kubwa maalumu kwa ajili yako wewe ambaye unapenda KURUDISHA TENA UKUU WAKO ULIOKUWA NAO lakini kwa sababu mbalimbali ukaja kukuponyoka, KUJIHUISHA TENA au KURUDISHA UWEZO ULIOKUWA NAO KWA MARA NYINGINE TENA. Nimeamua kuitumia kaulimbiu ya ushindi aliyoitumia Rais mteule wa Taifa la Marekani Bwana Donald Trump kuingia ikulu ya White House kwa mara nyingine tena kinyume kabisa na matarajio ya wengi baada ya ule ushindi wa mara ya kwanza kumponyoka.

Vivyo hivyo kinyume kabisa na matarajio ya wale wanaokufahamu na wanaodhania ya kwamba huu ndiyo mwisho wako na hautakaa uje uinuke tena watashangazwa na jinsi utakavyoweza kurudisha ukuu wako kwa mara nyingine tena. Kuwa tena mtu mwenye thamani mbele ya jamii, kuwa tena mtu unayejitegemea, usiyeombaomba kama ‘Matonya’, kuwa tena mtu wa ibada unayetii maagizo ya Mwenyezi Mungu na kurudi tena kuwa mtu mwenye malengo na msimamo usioyumbishwa ovyo na watu wenye pesa au mamlaka.

Kama unafuatilia vizuri makala zetu hapa utakumbuka nilianza kuizungumzia kampeni hii ya MAKE YOURSEL GREAT AGAIN mwezi November kabla hata Trump hajaonyesha dalili za kushinda uchaguzi wa 2025, na nikasema kwamba ashinde asishinde mimi siasa siyo kipaumbele changu bali sera zake juu ya uchumi na biashara, hivyo hata ikiwa asingeshinda bado kaulimbiu hii ingeendelea kama kawaida.

Pia kwa wanafunzi wangu hasa katika MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE nimekuwa kimya kidogo tangu mwezi Desemba na nilifanya hivi kwa madhumuni ya likizo lakini pia kuhakikisha kampeni yetu inaanza rasmi sambamba na kuapishwa rasmi kwa Rais Mteule Donald Trump tarehe 20 January 2025 ambayo pia ni siku ya kumbukumbu ya Mwanaharakati mwingine wa Marekani Martin Luther King Jr.

Kwahiyo kama wewe unayesoma hapa ni mwanafunzi wa Michanganuo-online nichukue nafasi hii kukuomba radhi kwa ucheleweshaji wa baadhi ya programu zetu hasa ile ya semina ya siku 7 ya Usagishaji unga wa Sembe & Dona lakini kukujulisha kwamba sasa tunakwenda kuuwasha tena moto upyaa! Na haijawahi kutokea toka group hili limeanzishwa.

Ikiwa uliwahi kuupoteza ukuu wako utaurudisha upya na pia ikiwa wewe ni kijana unayetamani kuujenga ukuu wako kwa mara ya kwanza utafanikiwa kuujenga kwani haimaanishi tunadili na waliopoteza ukuu wao tu bali hata na wale wanaotamani kuujenga kwa mara ya kwanza kabisa.

Trump ameapa kuijenga upya tena marekani (Make America Great Again), akimaanisha Marekani kuzidisha uzalendo mara dufu. Uzalendo maana yake ni kujali zaidi mambo yako na kuachana au kupunguza kuhangaikia ya watu wengine kwa madhumuni ya kujijengea uwezo mkubwa zaidi. Kwa mfano badala ya kufadhili vita kwenye nchi nyingine Marekani sasa itaelekeza nguvu na rasilimali zake nyingi kwenye kuujenga zaidi uchumi wake ili izidi kuwa na nguvu kwenye kila nyanja.

Na sisi kwa kutumia falsafa hii hii, tunaweza pia kutumia muda na rasilimali zetu kizalendo zaidi kusudi tuweze kujijengea uwezo mkubwa na wa haraka zaidi kiuchumi. Kwa mfano badala ya kuendelea kupoteza muda wetu wa thamani kujaribu kumridhisha kila mtu, jamaa na marafiki kwa masuala mengine ambayo hata hayana faida kwetu wala kwao ili tu eti wasituone wabaya, muda huo tunaweza kuutumia kikamilifu kukamilisha majukumu yetu mengine ya maana zaidi maishani ikiwemo kutafuta pesa.

Kampeni hii kama kampeni nyingine tulizoendesha huko nyuma kwa mafanikio makubwa mfano ile tuliyoibatiza jina, “KUELEKEAUTAJIRI” itaendeshwa kupitia Watsap, Telegram blog, vitabu na mitandao ya kijamii yote ya Self Help Books Publishers kwa njia mbalimbali zikiwemo makala, picha, video, na sauti.

Msomaji kwa kufuatilia kampeni hii utapata manufaa makubwa katika maisha yako siyo tu katika suala zima la biashara na ujasiriamali, bali hata na mtazamo wako kifikra katika maisha ya kila siku. Utajirudishia maisha yako yaliyokuwa yamejaa heri, fanaka na matumaini makubwa, maisha yaliyojaa mafanikio katika kila jambo unalolifanya.

Ili kwenda sambamba na kampeni hii nitakuomba ufanye mambo kadhaa, nasema nitakuomba kwa sababu ni hiari yako siyo lazima, unaweza tu kufuatilia kampeni bila kutimiza vitu hivyo na ikakusaidia lakini itakusaidia zaidi na utaona matokeo bora na chanya zaidi endapo utaweza kutimiza ombi ninalotaka kukuomba. Ombi lenyewe ni hili hapa chini,

1. Jitahidi sana upate hivi vitabu mashuhuri vinne kutoka Self Help Books Publishers vya elimu ya pesa, biashara, ujasiriamali na maendeleo binafsi) huwa napenda kuviita “The books of all Times” /vitabu vya wakati wote visivyopitwa na wakati kwani biashara itaendelea kuwepo muda wote binadamu atakaoishi duniani. Si lazima usome vyote ingawa ukipata vyote itakuwa bora zaidi, vitabu hivyo ni hivi vifuatavyo;-

(i) MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI

Kitabu cha kurasa 438 kwa lugha ya kiswahili kilichobeba masomo yote ya ujasiriamali na biashara pamoja na michanganuo halisi ya biashara na mawazo ya biashara zinazolipa zaidi ya 50.

(ii) THINK & GROW RICH-SWAHILI EDITION (Fikiri & Utajirike)

Fikiri na Utajirike cha Napoleon Hill ni Kitabu cha elimu ya fedha na mafanikio maarufu zaidi duniani na kimewahi kusomwa na watu zadi ya milioni 200. Kimetengeneza na kinaendelea kutengeneza mabilionea na mamilionea wengi zaidi duniani kuliko kitabu kingine chochote kile chini ya jua. Sasa hivi unaweza kujipatia nakala yako kwa Kiswahili sanifu ukasoma

(iii) SIRIYA MAFANIKIO YA BIASHARA YA REJAREJA

Kitabu kinachokupa muongozo kamili wa namna ya kufanya biashara yeyote ile ya rejareja kwa ufanisi wa hali ya juu. “Baadhi ya watu hudai eti, Duka halina faida, lakini usidanganyike, kwanini watu wasiyafunge na kila siku unayaona mapya yakifunguliwa? Gundua siri iliyojificha nyuma ya pazia kwa muda mrefu huku ukidanganywa biashara za rejareja hazina faida wakati wengine wakinunua magari, kusomesha watoto shule nzuri na hata kujenga majumba kwa biashara hizohizo.

(iv) MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA

Huwa nakiita kitabu cha maajabu kwani kitabu hiki kimebadilisha mno maisha ya watu wengi. Ukitaka kufahamu kama kitu ni kizuri basi utaona watu wakikazana kukiiga. Kitabu hiki nilichokitoa tangu mwaka 2012 kimeigwa na watu mbalimbali wengine wakiita vya kwao, Mifereji 9 ya pesa, Mifereji 10 ya kipatao nk. Lakini Kitabu Original ni ‘Mifereji 7 ya Pesa’ kilichoandikwa na Peter Augustino.

Kwa kifupi unaposoma kitabu hiki kama ulikuwa umeajiriwa unaweza siku hiyo hiyo ukaenda kumwambia bosi wako “Naacha kazi bosi nikaanzishe biashara yangu mwenyewe” Lakini nakusihi utakapokisoma usije ukadhubutu kufanya hivyo kwani unahitaji muda wa matayarisho kufanya jambo kama hilo na hata katika kitabu chenyewe mwishoni nimekuwekea tahathari hiyo.

(v) KANUNI YA KUJIFUNZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO (Toleo jipya 2024)

Umuhimu wa kitabu hiki utaujua baada ya kukisoma. 

2. Kitu kingine ninachokushauri kukifanya kusudi uweze kwenda na sisi sambamba katika Kampeni hii kubwa ya kihistoria ya Make yourself Great Again ni kujiunga na MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE-2025.

Tiketi ya kujiunga na familia hii ya kipekee kwa mwaka mzima ni kulipia kifurushi cha OFFA ya vitabu, michanganuo ya biashara na vitu vingine mbalimbali kwa shilingi elfu 10 tu! Orodha ya vitu hivyo imeongezwa mpaka kufikia vitu 20 kwa siku hizi 2 mpaka tarehe 20 itakapomalizika rasmi na ipo pale chini mwisho kabisa mwa makala hii.

Habari njema tu ni kwamba ikiwa utalipia kifurushi hiki, moja kwa moja pia utakuwa umejipatia vitabu nilivyovitaja pale juu kasoro vitabu viwili tu, cha Fikiri & Utajirike na kile cha Mafanikio ya biashara ya Rejareja.

Punde tu ulipiapo OFFA yako hii unatumiwa papo hapo vitu vyote 20 kisha kuunganishwa na MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE. Ukijiunga masomo na semina vinaanza siku hiyohiyo. Ndani ya group kuna programu mbalimbali utakazoshiriki ambazo ndizo kwa pamoja zitakazorudisha tena au kuujenga ukuu wako (Make yourself great), kubwa zikiwa ni hizi programu 5 zifuatazo;

                1)      Semina ya siku 7 (Seven Days Business plan Master class) – Semina hii mwanachama huanza hima siku anajiunga ambapo tunajifunza jinsi ya kuandika mchanganuo kamili na sanifu wa biashara yeyote ile kwa kutumia mfano halisi wa biashara mojawapo. Kwa sasa hivi tuko na biashara ya usagishaji wa unga wa Sembe na Dona.

                2)      Masomo ya mtiririko wa fedha (Cash flow classes) – Haya ni masomo ya kila siku yanayohusiana na nzunguko wa fedha binafsi na kwenye biashara zetu kwani biashara nyingi hufa si kwa sababu ya kukosa wateja bali kukosa mzunguko wa kutosha wa fedha.

                3)      Michanganuo bunifu mifupi mifupi ya biashara zenye fursa kubwa ya kutengeneza faida haraka- Hapa tutakwenda kujifunza mbinu, mikakati na ubunifu (Bootstrapping strategies) kwa ajili ya kukuza biashara ndogondogo haraka kwa mitaji kidogo. Ni maalumu kwa wale wafanyabiashara ndogondogo wasiokopesheka kirahisi na taasisi kubwa za kifedha, wanaotamani kutoka pale walipo na kusogea hatua kubwa zaidi ndani ya muda mfupi kadiri iwezekanavyo.

                4)      Biashara Shamba Darasa: Hii ni programu maalumu itakayohusu mafunzo kwa vitendo katika biashara ambazo tayari tumekwishafanya mazungumzo na wamiliki wake. Washiriki watapata fursa ya kuzifuatilia biashara hizo kwa picha na video huku na wao kama wakipenda wakiendesha biashara zakwao zinazofanana nayo sambamba na hiyo kwa ajili ya kupata matokeo sawa au bora zaidi. Wamiliki wa biashara hizo ni watu walionufaika na ushauri wetu kwa muda mrefu na kuridhika na matokeo wanayoyapata.  

                5)      Uchambuzi wa Kitabu Think & Grow Rich kwa Kiswahili- Mfasiri wa kitabu hiki kwa Kiswahili ni sisi wenyewe Self Help Books Tanzania, hivyo hapana shaka washiriki wa group hili watapata ladha halisi ya uchambuzi wa kina kutoka nakala Orijino isiyogushiwa aliyochapisha Napoleon Hill mwenyewe mnamo mwaka 1937

                6)      Washiriki watakuwa na fursa ya kujitangaza wao na biashara zao au shughuli wazifanyazo bila vikwazo visivyo na msingi- Mastermind group ni ushirika wa kusaidiana kila mmoja hivyo mtu akikosea tunarekebishana kistaarabu. Kundi litaongozwa kwa mtindo uliotumiwa na mwandishi NAPOLEON HILL kwenye madarasa na Semina zake katika Mastermind Group na Mikutano yake na washauri wasioonekaka kwenye kitabu cha Think & Grow Rich.

Wakufunzi huwa tunawahi darasani masaa 2 mpaka 3 kabla ya muda halisi kusudi kusuluhisha changamoto mbalimbali za wanafunzi wakiwemo wale waliochelewa kujiunga na semina au ambao hawakuelewa barabara somo lililopita.Tunakuwa tayari masaa yote hata nje ya darasa kusikiliza na kujibu maswali ya wanafunzi wetu

Ikiwa utafuatilia na kuzingatia vyema kampeni hii ya “KUJIRUDISHIA TENA UKUU WAKO” au “MAKE YOURSELF GREAT AGAIN” ya mwaka 2025, Sina shaka yeyote kwamba mwaka huu utakwenda kuwa wa Mafanikio makubwa na Baraka nyingi kwako. Anza mwaka kwa furaha na amani kama atakavyofanya Raisi Mteule wa Taifa la Marekani Donald Trump na familia yake, mkewe Melanie na wanawe, Donald Trump Jr. Ivanka, Eric na Barron.

..........................................

JINSI YA KUFANYA MALIPO (TZS 10,000/=)

Namba ya malipo ni; 0712202244 jina ni Peter Augustino Tarimo, kisha ujumbe sms au watsap usemao “NATAKA OFFA ISIYOWAHI KUTOKEA YA SIKU 2 TU” Mara moja nitakutumia zawadi zako zote 20 pamoja na kukuunganisha na MASTERMIND-GROUP letu la mwaka 2025

AU

Unaweza kuingia mwenyewe kwenye duka letu hili la mtandaoni la, Selar.co/augustinopeter na kulipia moja kwa moja sh. elfu 10 pasipo kuwasiliana hata na sisi ukitumia mtandao wowote ule wa simu unaotumia halafu utapewa kifurushi cha ZIP utakachodownload zawadi. Unzip kifurushi hicho na kutoa zawadi zako zote 20. Kisha nitakuunga mara moja kwenye MASTERMIND GROUP 

NB: Unaweza kunikumbusha kwa meseji nikuunganishe endapo nitachelewa kucheki mfumo wa selar.

*Kumbuka pia hii OFFA ya vitu 20 itadumu kwa siku 2 tu, tarehe 18 na 19 Januari 2025 kabla ya siku rasmi ya kuapishwa Donald Trump, na wanahitajika watu 20 tu kukamilisha idadi ya group la 2025 kabla hatujauwasha moto rasmi wa kampeni ya kujirudishia ukuu wetu tena, hivyo nakusihi chukua hatua mapema ikiwa utahitaji kuwa mwanafamilia ‘onboard’

HUDUMA ZETU NYINGINE

Mbali na vitabu, michanganuo na kampeni yetu hiyo kubwa pia tunayo huduma nyingine muhimu ya kuwaandikia wafanyabiashara na makampuni Michanganuo ya Biashara zao. Mpaka sasa hivi tumekwisha waandikia mamia ya watu na makampuni ‘Bplans’ zao. Baadhi yao tumeweka kwa kifupi mihutasari ya michanganuo hiyo (Executive summaries) bila kutaja utambulisho wao hapa: >>OUR PORTFOLIO>>. Bado tunaendelea kuorodhesha michanganuo zaidi ambayo hatukuwa tumeiweka hapo

Ikiwa unahitaji kuandikiwa mchanganuo wa biashara yako yeyote ile kubwa au ndogo, kuombea mkopo au kuendeshea tu biashara kwa ufanisi, basi tafadhali tunaomba hiyo kazi, tutakuandikia mpango-biashara unaoendana na maono yako halisi kwa gharama rafiki sana usiyoweza kuipata mahali pengine popote.

...........................................

Makala hii imeandaliwa na;

Peter Augustino Tarimo

Mtaalamu wa Michanganuo ya Biashara

Simu/sms: 0712202244

Watsap: 0765553030

 

ORODHA YA KIFURUSHI CHA OFFA ISIYOWAHI KUTOKEA YA SIKU 2 TU! (Tarehe 18 & 19 Januari 2025)

*Ukifanikiwa kuiona Offa hii tafadhali usimwambie mtu mwingine yeyote kwani akija kuikosa itakuwa lawama kwako bure.

Nikuibie tu siri kidogo..... Kuna vitabu na michanganuo hapa huwezi kuvipata mahali kwingine kokote na ukivikosa hapa kuvipata tena labda mwakani kipindi kama hiki.

VITU HIVYO 20 VYA OFFA NI HIVI HAPA;-

                  1.       KITABU: Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu za BIASHARA, jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika kila kitu.kwa kiswahili

                 2.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa kwa kiswahili

                 3.      KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.- kwa kiswahili

                 4.       KITABU: Njia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 tu! - kwa kiswahili

                 5.       KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ni maarufu sana duniani hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza

                 6.       KITABU: THE BOOK ON BUSINESS PLANNING- A step by step guide; cha mwandishi nguli wa michanganuo Tim Berry.-kwa kiingereza

                 7.       MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilers - kwa kiswahili

                 8.      MCHANGANUO: Kuku wa nyama-Tumaini Broilers .-kwa kiingereza

                 9.      MCHANGANUO: Poultry Production 5000 Broilers (Delicious Poultry Production) .-kwa kiingereza

              10.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant kwa Kiswahili

              11.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant kwa kiingereza

              12.    MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado milling) - kwa Kiswahili

              13.    MCHANGANUO: Kiwanda kidogo cha mvinyo na juisi ya Rosella -kwa Kiswahili

              14.    MCHANGANUO: Kiwanda kidogo cha kukoboa mpunga (Kikundi cha kina mama) - kwa Kiswahili

              15.    MCHANGANUO: Kiwanda cha kufyatua tofali za saruji (Kiluvya bricks) - kwa kiswahili

              16.    MCHANGANUO: Event planning and Management (Margareta Events in Dar)kwa kiingereza

              17.    MCHANGANUO: Biashara ya kuuza chipsi (Amani chipsi centre Buguruni)kwa Kiswahili

              18.    MCHANGANUO MFUPI: Biashara ya Steshenari (Neema Stationery)kwa Kiswahili

              19.    B/PLAN TEMPLATE (KIELEZO): kwa kiingereza

              20.    B/PLAN TEMPLATE(KIELEZO): kwa kiswahili

              21.    Kuunganishwa Mastermind Group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima(Mentorship group)

Namba ya malipo ni 0712202244 (Peter Auustino Tarimo). Lipia sh. elfu 10 kupata Offa hii sasa hivi na kuunganishwa Mastermind Group la Michanganuo kwa mwaka mzima wa 2025

0 Response to "JIRUDISHIE UKUU WAKO TENA (MAKE YOURSELF GREAT AGAIN) "

Post a Comment