BIASHARA YA GENGE, SHAMBA DARASA (PROGRAMU MAALUMU YA KIVITENDO ZAIDI) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BIASHARA YA GENGE, SHAMBA DARASA (PROGRAMU MAALUMU YA KIVITENDO ZAIDI)

Genge shamba darasa

Biashara ya Genge Shamba Darasa ni Programu maalumu miongoni mwa programu yetu mama ya mwaka huu wa 2025 ya JIRUDISHIE UKUU WAKO TENA (MAKE YOURSELF GREAT AGAIN, programu inayolenga kusisimua spirit/roho ya shauku kali ya kupata mafanikio kwa mara nyingine tena baada ya kuanguka mara ya mwanzo, lakini hata kupata mafanikio makubwa kwa mtu yeyote yule ambaye kwaza ndiyo safari yake ya mafanikio anaianza, hakuwa bado amewahi kufanikiwa hapo awali hasahasa vijana.

Programu ya shamba darasa maana yake ni mafunzo live’ ya moja kwa moja ya kivitendo yatakayohusisha biashara mbalimbali zitakazotumia ubunifu mkubwa katika kuzifanikisha. Ubunifu huo utaziwezesha biashara hizo kuzalisha faida kubwa na kwa haraka licha ya kuwa ni biashara za mtaji kidogo.

Tutakachofanya sisi kama wakufunzi na wahamasishaji wa biashara na ujasiriamali ni kujenga urafiki/ukaribu na wamiliki wa biashara hizo kwa kuwapatia ushauri na hata wakati mwingine usimamizi wa karibu kwenye biashara zao kusudi wakubali biashara hizo kutumika kama mifano (Shamba Darasa) kwa ajili ya kufundishia kivitendo wanafunzi wengine walio na biashara kama hizo zinazosuasua ama wale wanaotamani siku moja kuja kumiliki biashara zinazofanana zazo.

Tumeamua rasmi sasa kuhama kutoka kwenye mafunzo ya nadharia kuja kwenye mfumo huu wa kufundisha kivitendo zaidi

Wanafunzi watakaopenda kujiunga na programu hii watalipia ada kidogo tu kwa ajili ya kujipatia moja kati ya vitabu vyetu 2, cha Genge la matunda na mbogamboga na kile cha Mafanikio ya biashara ya Duka la Rejareja .

Punde tu baada ya malipo atatumiwa kitabu pamoja na kuunganishwa magroup ya Watsap na Telegramu. Kwanini magroup mawili? Group la Telegramu tumeliweka kwa madhumuni ya kuhakikisha kila mwanachama mpya anayejiunga anapata mfululizo wa matukio yote tangu yanaaza mpaka yalipofikia tofauti na watsap ambayo huanza pale tu unapojiunga.

Ndani ya shamba darasa shughuli kubwa itakuwa ni kujifunza hatua kwa hatua jinsi biashara halisi inavyoanza na kuendelea siku hadi siku. Kila siku tutakuwa tukiripoti maendeleo ya biashara na matukio yote bila kukosa tukitumia data/taarifa watakazotupatia wamiliki wa biashara husika, data ambazo bila shaka yeyote ile zitakuwa ni sahihi, halisi na zinazoendana na wakati.

BIASHARA YA GENGE SHAMBA DARASA

Tayari nimeshazungumza na wajasiriamali kadhaa na baadhi yao wamenikubalia kutumia biashara zao kama Shamba Darasa la kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wengine walio na shauku kali ya kufanikisha biashara zao kama hizo huku na mimi pia nikiendelea kutoa ushauri kwao wa kitaalamu na kiubunifu wa namna watakavyoweza kuziboresha biashara hizi ziweze kuwazalishia mapato makubwa ya uhakika na hatimaye waweze kumiliki mitaji mikubwa na ya maana zaidi.

Kwa kuanza tuna biashara moja ya Genge la matunda na mbogamboga mchanganyiko na Vyakula vya kuku, Pumba na Mkaa. Biashara hii inamilikiwa na mtu mmoja aitwaye Swai, (hajapenda niweke hapa utambulisho wake kamili), ndio maana nitatumia tu jina lake la ubini, Swai. Biashara ipo katika eneo la Temboni Kimara Dar es salaam karibu na kituo kidogo cha polisi Temboni. Ni biashara inayoanza ingawa hapo awali palikuwa na mmiliki mwingine ambaye baada ya kuhama alimuuzia mmiliki mpya baadhi ya bidhaa na vifaa vilivyokuwemo pale. Banda pia ni la kukodi na kwa mwezi kodi ya pango ni shilingi 20,000/=

Binafsi nimehusika moja kwa moja katika kutoa ushauri wakati wa uchaguzi wa eneo hili la biashara ya genge la Bwana Swai, nilimshauri pia jinsi ya kuandaa madaftari ya kuweka kumbukumbu na hesabu za biashara yake ili kufahamu maendeleo yake kila siku ikiwa anapata faida kiasi gani na anatumia kiasi gani pia.

Si hivyo tu bali nilimuandalia na mpango mfupi wa biashara yake (Mchanganuo mfupi wa biashara) ili kufahamu kiasi cha mahitaji yake kulingana na kiasi cha fedha/mtaji aliokuwa nao na mazingira mazima ya wateja katika eneo alilochagua kuweka hili genge lake. Kumbuka alikuwa na mtaji kidogo sana hivyo ilibidi tuanze na vile vitu muhimu zaidi tu vilivyohitajika ili biashara iweze kuanza.

Nilimwambia Swai  ufinyu wa mtaji hilo ni tatizo la muda mfupi tu na asijali, ukizingatia eneo lenyewe tulishabaini kuwa ni ‘potential’ (yaani lina uwezekano mkubwa wa kuja kulipa hapo baadae) Kilichohitajika hapa ni mbinu tu za kufunga mkanda kisawasawa (Bootstrapping strategies)

Swai alikuwa na mtaji fedha kiasi cha shilingi laki mbili na elfu ishirini na moja tu, 221,000/= ambapo kiasi cha shilingi 26,000/= alitumia kulipia baadhi ya bidhaa alizoacha mmiliki wa zamani wa genge na shilingi 195,000/= kwa ajili ya kwenda kununulia bidhaa nyingine mbalimbali mpya kwa bei ya jumla sokoni

Kwa upande wa vifaa na mali nyinginezo za kudumu mfano mzani na fenicha alichukua baadhi ya vitu kutoka nyumbani kwake na vingine aliachiwa na mmiliki wa zamani, hata hivyo vifaa na mali hizo tumezithamanisha jumla yake kuwa ni shilingi 153,000/= Kwa hiyo utaona ya kwamba Genge la Bwana Swai lilianza na jumla ya Rasilimali zenye thamani ya shilingi 374,000/= tu kama ‘screenshot’ ya daftari lake la Mali za biashara za kuanzia inavyoonyesha hapo chini;

Daftari la mali za biashara

Biashara ilianza rasmi siku ya tarehe 11/02/2025 akanishirikisha na nilimpatia ushauri kadiri alivyohitaji. Kwanza nilimsihi anunue zile bidhaa tu zilizokuwa na uwezekano wa kutoka haraka na anunue kiasi kidogokidogo sana mpaka atakapofahamu ni zipi zinazotoka haraka zaidi na kwa kiasi gani. Baadhi ya bidhaa mfano zile za gharama ya juu sana nilimshauri kabisa asinunue asubiri mpaka pale mzunguko wake wa fedha utakapotengemaa na mtaji kukua kidogo.

Tangu siku hiyo ya kwanza alinishirikisha madaftari yake yote ya kuweka kumbukumbu likiwemo Daftari la Mali za biashara, Daftari la Manunuzi ya biashara, Daftari la Mauzo ya biashara na Daftari la Matumizi ya biashara. Nilimshauri kutumia madaftari 4 badala ya 3 kama ilivyosisitizwa kwenye kitabu chetu toleo jipya la 2025 kwani Swai hana mfanyakazi anauza tu mwenyewe gengeni kwake.

Mfumo maalumu wa madaftari 3 au mfumo wa Daftari moja tu ni mahsusi kwa ajili ya wale tu ambao malengo yao ni kuthibiti mahesabu wasaidizi wasiwe na uwezo wa kuwaibia au kufanya hujuma zozote nyingine kirahisi, ukisoma ndani ya kitabu hicho maelezo yake yanajitosheleza. Ni mifumo ambayo huhitaji mambo mengi na unaweza kuwa na madaftari mengine manne kwa ajili yako binafsi ila mfanyakazi yake ni 3 tu au moja basi mmemaliza.

Kwenye magroup ya Watsap na Telegramu ya Genge Shamba Darasa kuanzia leo nitaweka mfululizo wa kumbukumbu zote kwenye haya madaftari manne tangu siku ya kwanza genge hili linaanza.Washiriki watapata fursa ya kujua kwa mfano kila siku zilinunuliwa bidhaa za shilingi ngapi na matarajio ya faida kwa bidhaa zote zilizonunuliwa kila siku ni kiasi gani.

Halikadhalika watafahamu kila siku genge linauza bidhaa zipi, bei ya kila bidhaa iliyouzwa, jumla yake na jumla kuu ya mauzo ya siku husika. Watafahamu pia kila matumizi yaliyofanyika siku hiyo na jumla yake.

Kumbukumbu hizi nitaendelea kuziweka hata baada ya siku ya leo kwani haitarajiwi biashara hii kufikia ukomo siku za karibuni, ni zoezi la muda mrefu na washiriki watanufaika pakubwa kuona maendeleo yake itafika wapi. Je Biashara ya Swai itafanikiwa au itafika mahali itafeli?

Madaftari haya 4 yatawezesha siku yeyote kujua ikiwa mtaji wa biashara umeongezeka kwa kiasi gani ama kupungua na ongezeko au upungufu huo umetokana na sababu gani kulingana na rekodi zilizowekwa. Yatamsaidia pia Bwana Swai kufanya maamuzi baada ya kipindi chochote kile ikiwa aendelee na biashara hii inalipa ama aamue kuachana nayo mazima kwa kuwa hailipi akatafute mishemishe zingine mjini.

Ikiwa wewe ni mfanyabiashara/mjasiriamali yeyote yule wa biashara ya rejareja, duka, kioski, genge, nguo, duka la dawa au hata vifaa vya ujenzi, programu hii siyo ya kukosa kwani ndani ya group hili licha ya kufuatilia mwenendo wa Genge hili la Bwana Swai lakini pia tutajadili na kujibu swali lolote lile kuhusiana na yale yote yaliyoandikwa ndani ya kitabu cha Mafanikio ya Biashara ya Duka la Rejareja & Genge ndani yake Toleo jipya 2025

Na maswala mengine yote kuhusiana na Biashara za rejareja, changamoto, mafanikio, mbinu na mikakati kadha wa kadha mfano ile ya kufunga mkanda (Bootstrapping), ubunifu na matumizi ya Akili bandia/Akili mnemba (AI) na mifumo mingine katika kuleta ufanisi kwenye biashara yeyote ile ya rejareja hata ikiw unauza ubuyu wa kufunga.

JINSI YA KUJIUNGA NA PROGRAMU YA GENGE SHAMBA DARASA

Kujiunga na programu ya Genge shamba darasa, lipia moja kati  cha MAFANIKIO YA BIASHARA DUKA LA REJAREJA sh. 6,000/=  au kile cha GENGE LA MATUNDA & MBOGAMBOGA 2025, shilingi 5,000/= kupitia namba 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo na kisha ujumbe, “NATAKA PROGRAM GENGE SHAMBA DARASA”, nitakutumia kitabu chako mara moja kwenye simu au kompyuta yako na kukuunga na magroup yote 2

Unaweza pia kununua vitabu hivi moja kwa moja kupitia duka letu la SELARKWA KUBOFYA HAPA, lipia kwa mtandao wako wa simu unaotumia na upakue kitabu muda huohuo kisha nitumie ujumbe au nitakuona mwenyewe moja kwa moja katika mfumo wa selar na kukuunga na magroup

Ukinunua nakala ngumu ya kitabu (Hardcopy) Unapewa offa vitabu vyote 2 kwa pamoja na kuunganishwa kwenye magroup kama kawaida. Bei ya nakala ngumu vitabu vyote 2 kwa Dar es salaa ni sh. 25,000/= tunakuletea mpaka pale ulipo, na Mikoa mingine (mkoa wowote ule) kwa njia ya Basi ni shilingi 30,000/=

MAWASILIANO YETU NI:

Simu/sms: 0712202244

Watsap:     0765553030

 

BONUS-PROGRAM

Ikiwa utalipia programu hii kabla ya tarehe 25/02/2025 utapata bure programu nyingine ya Shamba darasa iitwayo; MAAJABU YA MBOGA YA CHAINISI SOKONI. Chinese/Chainisi ni mboga yenye asili yake huko Uchina lakini inalimwa sana hapa Tanzania na ni mboga maarufu mno katika kila soko na magenge yote mitaani mijini na vijijini.

Maajabu ya mboga hii ni kwamba humpatia faida nzuri sana kila anayejihusisha katika mnyororo wake mzima wa uzalishaji, mkulima, muuzaji jumla (dalali), muuzaji rejareja na hata mlaji wa mwisho. Woote hao ‘huenjoy’ faida za chainisi kwa namna ya kushangaza sana!

Kitu kingine cha kipekee sana nilichoweka kwenye hii programu ni ubunifu mkubwa katika uzalishaji wa mboga hii uliorahisishwa ! Tutazalisha Chainisi hatua kwa hatua ndani ya Group letu la Maajabu ya Chainisi Sokoni kwa kutumia njia za kiubunifu zisizowahi kutumika mahali pengine popote pale tukitumia kwa mara ya kwanza kabisa Greenhouse ya kienyeji isiyohitaji gharama kubwa ambapo chainisi zitalimwa majira yote ya mwaka iwe mvua iwe kiangazi huku mavuno yakiwa makubwa muda wote

Kwa kuanza tayari nimeshaandaa kitalu kwa ajili ya kusia mbegu na tutazalisha Chainisi kwa wingi hata katikati ya msimu huu ujao wa masika miezi ya 3 mpaka 6 wakati ambao wakulima wengi hulalamika mavuno kidogo shauri ya mvua nyingi, sisi mvua kwetu haitakuwa ‘ishu’ Kwa kutumia mbinu tulizobuni wenyewe na kuzithibitisha utalima Chainisi hata kama unaishi eneo linanojaa maji muda mrefu kama pale Mtaa wa Jangwani Kariakoo karibu na club ya Yanga.

 

PROGRAMU & HUDUMA ZETU NYINGINE

1. MICHANGANUO-ONINE MASTERMIND GROUP

Programu hii bado inaendelea kila siku kwa wale wote wanaohitaji kujifunza jinsi ya kuandaa Michanganuo ya biashara zao au kuwa wataalamu/experts kwenye uandishi wa Michanganuo ya biashara (Master Class). Ndani ya group pia kunapatikana masomo ya mtiririko wa fedha kwenye biashara (Cash flow Subjects) na Michanganuo bunifu ya biashara ndogo ndogo zinazolipa faida kubwa haraka

Kiingilio ni kulipia Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI sh. 10,000/= na kisha unapata OFFA/BONUS ya vitabu vingine na michanganuo jumla vitu 20, hii offa itamalizika muda siyo mrefu ndani ya mwezi huu huu wa February. Unaweza kulipia offa hii kupitia duka la selar na kudownload kifurushi cha Offa yako pasipo hata kuwasiliana na mimi kwanza, bofya hapa>>OFFA INAYOKARIBIA KUISHA MUDA WAKE

2. HUDUMA YA KUANDIKIWA MPANGO KAMILI WA BIASHARA YAKO KITAALAMU

Tunaomba kazi ya kukuandalia mchanganuo wa biashara yako yeyote ile iwe kubwa au ndogo kulingana na mahitaji yako wewe mwenyewe na soko lako kwa gharama rafiki. Tayari tumewaandalia makampuni na watu wengi binafsi mipango ya biashara zao na badhi yake unaweza kutazama mihutasari yake hapa>>BAADHI YA KAZI ZETU,

Karibu tupo kwa ajili yako!

Simu/sms: 0712202244

Watsap: 0765553030

3. NAKALA YA KITABU CHA THINK & GROW RICH KWA KISWAHILI (Fikiri & Utajirike)

Lipia sh. 10,000/=  kupitia Simu Janja yako kutoka app ya GETVALUE kwa kujisajili kupitia kiungo hiki >>Fikiri & Utajirike

 

 

HAWA NI BAADHI YA WADAU WALIOJIPATIA HUDUMA NA PROGRAMU ZETU

Mdau 1

Mdau 2









Makala imeandaliwa na:

Peter Tarimo

Mjasiriamali & Mtaalamu wa Michanganuo ya Biashara

Simu/sms: 0712202244

Watsap:  0765553030




SOMA NA HIZI HAPA;

 

                 1.       Siri 10 alizotumia aliko dangote tajiri namba1 afrika kutajirika

                 2.       Shauku: mwanzo wa mafanikio yote (hatua ya kwanza kuelekea utajiri)

                 3.       Kutafuta soko la bidha zako, kunahitaji ubunifu

                 4.       Hatua 7 rahisi za kuanzisha biashara yako ndogo ukiwa bado kazini umeajiriwa

                 5.       Kufa au kuanguka kwa biashara yako ndogo fanya vitu hivi 9 kujiepusha

                 6.       Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado-1

                 7.       Biasharaya kuuza dagaa mchele na samaki wa majichumvi kiubunifu: mchanganuo

0 Response to "BIASHARA YA GENGE, SHAMBA DARASA (PROGRAMU MAALUMU YA KIVITENDO ZAIDI)"

Post a Comment