Swali hili ikiwa kama biashara ya genge la matunda na
mbogamboga ina faida nusu kwa nusu nimekuwa nikikutana nalo mara nyingi lakini
nikawa nakwepa kulijibu moja kwa moja kutokana na sababu kubwa kwamba sikuwa
nimewahi kufanya utafiti wa kina kuhusiana na biashara hii.
Watu huhusianisha au kuifananisha biashara ya genge na
biashara nyingine ya duka la rejareja ambayo tayari nilikwishaifanyia utafiti
na kuandika kitabu chake siku za nyuma. Kiukweli ijapokuwa biashara hizi mbili
genge na duka zote ni biashara za rejareja na zina mambo mengi ya kufanana
lakini pia zina tofauti kadhaa
Mmoja kati ya waliowahi kuniuliza swali hili ni Bwana
Jackson wa Tegeta jijini Dar es salaam aliyeuliza kama ifuatavyo kupitia
mtandao wa watsap;
“Mtaalamu
nimekuwa nikifuatilia sana makala zako kuhusu biashara ya duka la rejareja
lakini mimi nataka nianze kwanza na genge la matunda na mbogamboga shauri ya
mtaji nilio nao kuwa kidogo mno, sasa ningependa kufahamu, hivi eti biashara ya
genge faida yake ni nusu kwa nusu ukinunua kitu shilingi 100 unakwenda kupata
faida shilingi 100 juu yake?”
Swali hili lilinisukuma kuanza kufanya utafiti mkubwa
kuhusiana na biashara hii ya genge la matunda na mbogamboga kwani kama
nilivyotangulia kusema ni biashara inayoshabihiana na ile ya duka la rejareja
ambayo tayari nazielewa ‘ABS’ zake
Mimi naishi Mbezi ya Kimara jijii Dar es salaam hivyo
nilianzia hapahapa Mbezi Temboni jirani kidogo na stendi ya mabasi. Nikamtafuta
mmiliki mmoja wa genge la matunda na mbogamboga nikajenga naye ukaribu
ulioniwezesha kuijua biashara hii kwa undani kabisa.
Mmiliki wa genge hili huchukua bidhaa zake hasahasa
katika soko la Mabibo lililopo karibu na Manzese lakini pia mara chache huenda
masoko ya Mbezi mwisho, Buguruni na Temeke Sterio kwa baadhi ya bidhaa. Kwahiyo
siku moja nikaongozana naye moja kwa moja mpaka Mahakama ya ndizi Mabibo, soko
lililopo jirani na kituo cha daladala cha Big Brother
Alinionyesha jinsi wanavyonunua bidhaa, nikatafiti bei za
matunda na mbogamboga pamoja na kufanya kila kitu nilichohitaji kufanya katika
ule utafiti wangu. Kwa kweli nilizifahamu siri nyingi sana za biashara ya genge
ambazo kukosa kufanya utafiti huu nisingeliweza kamwe kuzifahamu.
MAJIBU:
Ndugu yangu Jackson, mtu asikudanganye kuwa eti biashara
ya genge la matunda na mbogamboga bidhaa zake zote zina faida nusu kwa nusu
hapana, isipokuwa tu ni kweli kwa ujumla bidhaa za genge faida yake ni kubwa
kidogo ukilinganisha na bidhaa kwenye biashara ya duka la rejareja.
Ni ukweli usiopingika kwamba kuna baadhi ya bidhaa za
genge(chache) ukiuza unapata shilingi kwa shilingi nikimaanisha faida ni nusu
kwa nusu lakini siyo zote na utakapotafuta wastani utakuta kwa biashara nzima(bidhaa
zote kwa pamoja) faida haiwezi ikawa nusu kwa nusu shauri ya bidhaa nyingine nyingi
faida yake kuwa chini.
Kwenye duka la rejareja kwa mfano imethibitishwa kwamba
wastani wa faida ghafi kwa mauzo ya bidhaa ni asilimia 25% - 30% maana yake kwa
kila mauzo ya shilingi 100 unapata faida wastani wa shilingi 25 mpaka 30
Katika utafiti wangu nilioufanya Temboni asilimia ya
faidaghafi kwenye mauzo ya bidhaa za genge kwa wastani nilikuta ni asilimia 30% mpaka asilimia 35%. Hii inamaanisha kwamba
katika kila mauzo ya shilingi 100 faida ghafi ni wastani wa shilingi 30 mpaka
35. Kumbuka faida ghafi maana yake ni faida kabla hujatoa gharama za kudumu za
uendeshaji, kodi na riba.
Huu ni utafiti nilioufanya mwenyewe binafsi na si wa
kusoma mahali. Katika mfululizo wa makala zangu hizi maalumu kwa ajili ya genge
nitakuja kuelezea kwa mifano halisi jinsi nilivyokokotoa hii asilimia 30% mpaka 35% kama faida ghafi
Katika makala hizo zijazo pia nitazitaja baadhi ya bidhaa
za genge ambazo unapozinunua sokoni unakwenda kupata faida pasu kwa pasu
nikimaanisha faida ni nusu kwa nusu ama ukinunua shilingi mia unakwenda kuiuza
mia mbili, hivyo usikose kufuatilia blogu yako hii ya jifunzeujasiriamali
kila siku msimu huu wa genge la matunda na mboga.
Ijapokuwa nimesema kwenye genge kuna baadhi ya bidhaa
unapata faida nusu kwa nusu lakini haimaanishi kwamba faida ya genge zima kwa
wastani ni nusu kwa nusu pia hapana, kuna bidhaa nyingine nyingi zina faida
kidogo na hivyo kusababisha wastani wa faidaghafi nzima ya genge kuwa hiyo
asilimia 30% mpaka 35%
Sababu kubwa inayofaya iwe vigumu kuuza kila bidhaa ya
genge kwa bei mara mbili ya ile uliyonunulia ili faida ghafi iwe nusu kwa nusu ni
ushindani mkali. Wakati wewe unanunua papai shilingi elfu moja kwa bei ya jumla
na kutaka kwenda kuliuza shilingi elfu mbili kwa bei ya rejareja ili upate
faida nusu kwa nusu, mshindani wako pembeni mwenye genge kama lakwako yeye
anauza papai kama hilohilo kwa shilingi 1,500/= pekee
Utaona yakwamba mshindani wako huyu atauza na wewe mapapai
yako yatakudodea hutapata wa kumuuzia ng’o, na utalazimika tu hatimae na wewe
kuuza shilingi 1,500 au vinginevyo basi chini ya hapo kusudi uweze kwenda na
hali halisi ya soko lilivyo
Biashara za rejareja kwa ujumla huwezi ukaweka kiasi
kikubwa sana cha faida kufikia nusu kwa nusu faida, tazama bishara mfano Supermarkets huwa wanaweka faida kidogo
sana mpaka wakati mwingine kufikia hata asilimia 1% ya faida halisi kwa mauzo (profit margin), baada ya kutoa gharama zote. Lakini
wanachojivunia zaidi wao ni mauzo mengi (mass
sales).
Ukiuza kwa wingi sana hata kama unapata faida kidogo sana
kwa kila bidhaa hamna tatizo kwani ile faida kidogokidogo ikilundikana inakuwa
kubwa haraka, na supermarket kwa kuwa wana bidhaa nyingi mchanganyiko hii faida ya asilimia 1% inawatosha kwani kwa
siku ni mamilioni ya shilingi
Ripoti
kamili ya utafiti wa biashara ya genge la matunda na mbogamboga
Ripoti nzima ya utafiti wangu huu wa biashara ya genge la
matunda na mbogamboga ipo tayari na nimeiweka ndani ya kitabu cha BIASHARA YA GENGE LA MATUNDA & MBOGAMBOGA.
Kama kawaida hatujaacha kitu chcohcote ni Ripoti kamili. Ikiwa unataka
kuanzisha genge au tayari unalo tafadhali usiache kujipatia madini haya adimu
utakuja nishukuru baadae
Kitabu hiki kipya cha Biashara ya Genge la Matunda na Mbogamboga bei yake ni shilingi 5,000/= nakala tete (Softcopy) wakati kile cha Duka la rejareja bado ni shilingi 6,000/=
Vitabu hivi viwili siyo kwa walio na duka au genge tu hapana, vinafaa hata kwa yule anayefanya biashara nyingne yeyote ile ya rejareja.
Vitabu hivi 2 kwa ajili ya biashara za rejareja
unaweza kujipatia kwa urahisi muda wowote kwenye simu au kompyuta yako kwa
kufanya malipo kupitia nambari 0712202244
Peter Augustino Tarimo, kisha nitumie
ujumbe wa sms kwa namba hiyohiyo au watsap kwa namba, 0765553030 na
nitakurushia kitabu/vitabu vyako muda huohuo
AU
Unaweza pia kununua vitabu vyako moja kwa moja bila hata
ya kuwasiliana na sisi katika duka letu la mtandaoni la Selar kwa kutumia viungo vifuatavyo hapo chini; (Bonyeza kulipia moja kwa moja kwa kutumia
mtandao wako wa simu, Tigo(Yas), Voda au Airtel:)
1. BIASHARA YA GENGE LA MATUNDA & MBOGAMBOGA 2025: BEI = 5,000/=
2. DUKA LA REJAREJA
TOLEO JIPYA 2024 : BEI = 6,000/=
NAKALA NGUMU (HARDCOPY) YA KITABU CHA GENGE LA MATUNDA NA MBOGAMBOGA 2025 TUNAKULETEA MPAKA ULIPO DAR ES SALAAM KWA SH. 25,000/=. UNAPATA BURE NA KITABU CHA DUKA LA REJAREJA
PIA UNAPONUNUA KITABU CHA DUKA LA REJAREJA NAKALA NGUMU (HARDCOPY) SH.25,000/= TUNAKUPATIA NA KITABU CHA GENGE BURE BILA MALIPPO
MIKOA MINGINE PAMOJA NA ADA YA BASI NI SH. 30,000/=
.......................................
“Karibu ufanye mapinduzi makubwa kwenye biashara
yako ya rejareja mwaka huu wa 2025 haijalishi ni duka la vyakula, nguo, dawa,
genge au tu unauza ubuyu wako kwenye meza sokoni.”
Peter A. Tarimo
0712202244 / 0765553030
SOMA NA
HIZI HAPA;
Mchanganuo wa biashara ya genge la kisasa la matunda,
mbogamboga na vyakula
Siri ya kufanikiwa biashara ya kuuza vinywaji baridi vyenye
faida ndogondogo
Biashara ya mtaji wa million
mbili (2) ninayoweza kufanya ni ipi? naomba msaada
Biashara
bunifu za mtaji mdogo zinavvyoweza kukutoa kimaisha mwaka huu
Orodha ya biashara za vijijini unazoweza kuanza na mtaji wa sh.
laki 3 (300,000/=)
0 Response to "ETI NI KWELI BIASHARA YA GENGE LA MATUNDA NA MBOGAMBOGA INA FAIDA NUSU KWA NUSU?"
Post a Comment