Huu ni mwezi Aprili katikati kuelekea Mei lakini siyo
ajabu kukuta idadi kubwa ya watu waliokuwa na shamrashamra za kujiwekea malengo
kadha wa kadha ya kifedha pale Januari wameshasahau ama kuachana na malengo
hayo kitambo
Somo
hili ni moja kati ya mfululizo wa masomo mengine mengi yaliyo na maudhui
yahusuyo mzunguko wa fedha kwenye Mastermind Group la Michanganuo-online kila
siku.
Kwa kipindi kirefu watu wamekuwa na mitazamo tofauti
kuhusu suala la uwekaji wa malengo ya mwaka hususani malengo yale ya kifedha ya
muda mrefu mfano malengo ya mwaka, miaka 2, miaka 5 na wakati mwingine hata
malengo ya Milenia.
Ni jambo ambalo limekuwa likiwasumbua watu wengi kutokana
na ukweli mchungu kwamba, uwekaji wa malengo ya kifedha au kimaisha ni kitu
kimoja na utekelezaji wake ni kitu kingine tofauti kabisa
Katika malengo uliyojiwekea Januari ikiwa hautajifanyia
tathmini ya mara kwa mara huku ukirekebisha pale ambapo umetoka nje ya mstari
wa malengo yako ni dhahiri kabisa kwamba Desemba itafika na kukukuta hakuna cha
maana ulichotimiza.
Nimegundua kwamba unapokuwa na lengo kubwa ulilojiwekea
na litakalochukua muda mrefu kulitimiza tuseme labda miezi, mwaka nk. adui
namba moja atakayekuzuia usilitimize ni wasiwasi, ile hali ya kuwa na
mashakamashaka.
Unajisemea, “Ngoja niache leo nitafanya kesho”, eti
ukisubiria mpaka siku utakayokuwa katika ‘mudi’ nzuri ya kulitekeleza au utakapokuwa
na hamasa ya kutosha.
Nasema hivyo kwani wataalamu wanakuambia lengo lolote
lile kubwa ni lazima ulitimize kidogokidogo kila siku na hili halina ubishi
kabisa vinginevyo hautaweza kulitimiza hata ungepewa muda wa karne moja.
Watu mara nyingi tumekuwa tukiingia kwenye mtego wa kukaa
tukibweteka na kuanza kuwaza ni kwa jinsi gani tutakavyofurahia (kuenjoy) siku tukitimiza
malengo yetu badala ya kuutumia muda huo kufikiria ni nini cha kufanya ili
kutimiza malengo tuliyojiwekea kwa uendelevu.
Kwa hiyo msingi mkuu utakaokufanya hatimaye kuyafikia
malengo uliyojiwekea Januari ama kipindi kingine chochote kile cha mwaka
haijalishi ni lazima iwe uliyaweka mwezi Januari ni mazoea ya kutimiza lengo
lako kidogokidogo.
Katika somo letu hili la leo hivi punde, nitakwenda
kukutajia vitu vitano muhimu sana na vilivyokuwa na nguvu (very powerful) ambavyo ikiwa utakwenda kuvitia kwenye matendo basi
utaachana kabisa na kilema cha kughairisha utekelezaji wa malengo yako muda
mfupi tu baada ya kuyaweka..............
..........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
Ndugu
msomaji wangu, somo hili kamili tutajifunza leo kwenye Mastermind group la
Michanganuo-online.
Kujiunga
na group mwanachama anapaswa kununua kitabu cha Michanganuo ya Biashara & Ujasiriamali ambacho bei yake ni
shilingi elfu 10 kwa ajili ya rejea ya masomo mbalimbali atakayojifunza mwaka
mzima.
Baada
ya kujiunga unaweza kuaccess / kuyapata masomo mengine yote yaliyopita katika
channel yetu ya Telegramu pamoja na programu nyingine za kampeni ya “2025 MAKE YOURSELF GREAT AGAIN”, hivyo
unapaswa pia kuwa na account Telegram
Mawasiliano:
Watsap/Call: 0765553030
Namba ya kulipia: 0761002125
Peter Augustino
Baada ya malipo tuma ujumbe “NIUNGE MASTERMIND GROUP LA
MICHANGANUO 2025”
SOMA
NA HIZI PIA:
1. Maajabu ya kufikiri mambo makubwa na kwanini uweke malengo
makubwa maishani
2.
Biashara 7
nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala.
3. Ijue falsafa ya kitabu iliyotengeneza matajiri & mabilionea wengi
zaidi duniani
4. Mafanikio na utajiri wa watu wengi umetokana na falsafa hizi 7 za fedha
6. Wanaofanikiwa maishani wengi husema ‘no’(hapana) kwa vitu hivi 3
0 Response to "MALENGO YAKO KIFEDHA 2025, JE UNAYATIMIZA KAMA ULIVYOYAPANGA JANUARI IKIWA NI ZAIDI YA ROBO MWAKA SASA?"
Post a Comment