Ni picha gani inayokujia akilini unaposhuhudia harusi nzuri ya kupendeza kama hii pale Maharusi wakiwa na nyuso zilizojaa tabasamu wanapovishana pete au kulishana keki?
Kabla ya siku yenyewe ya ndoa kulikuwa na mchakato mrefu
kuanzia pale ndugu, jamaa na marafiki toka pande zote mbili, kike & kiumeni
walipoanza kukaa vikao vya kupeleka barua, mahari na kuvishana pete ya uchumba.
Kisha vikafuata vikao vya harusi na sendoff sambamba na
kuundwa kwa kamati za sherehe ambapo ndugu jamaa na marafiki hapa kila mmoja ‘akapledge’
kile alichofikiri atamudu kuchangia.
Hapa sasa ndipo kiini chenyewe hasa cha sherehe ya harusi
kilipo kwani bajeti inaanza kutengenezwa kulingana na kiasi cha fedha kilichokuwa
kikitolewa na wadau
Mchakato wote huo uliochukua takribani miezi kadhaa unaweza ukauita MIPANGO ya harusi na ndio msingi halisi wa sherehe yeyote ile ya harusi kupendeza.
Ikiwa kama mipango ilikuwa mibovu harusi haitapendeza lakini mipango ikiwa madhubuti na mizuri harusi hufana na watu kufurahia kama hii.
Si harusi tu peke yake bali hata na shughuli nyinginezo karibu zote binadamu tunazofanya ikiwemo BIASHARA, huhitaji mipango au maandalizi kabambe kabla ya matukio yenyewe halisi kufanyika.
Ukitaka biashara yako ishamiri na kukupatia faida kubwa
basi huna budi kufanya mipango kabla ya kuianza. Na si unapoanza tu bali hata
na biashara ya zamani unaweza pia kuiwekea mpango wa kuifufua au kuifanya iweze
kutengeneza faida kubwa zaidi ya ile uliyozoea.
Katika biashara watu wengi tumezoea kupanga tu wenyewe
kichwani na kuanza utekelezaji jambo ambalo si baya, lakini kuna kupanga na
kisha ukaiweka mipango yako kwenye karatasi jambo ambalo ni zuri zaidi na
linalozidisha mara dufu uwezekano wa biashara kufanikiwa kulingana na maelezo
ya wataalamu.
Kuandaa mpango wa biashara kuna faida nyingi kubwa ikiwa
ni kumfanya mjasiriamali aumize kichwa kuufikiria mchakato mzima wa biashara
yake jinsi utakavyokwenda na hivyo kupunguza uwezekano wa kuja kufanya makosa
mbalimbali mbele ya safari
Ni sawa na mtu kujifunza biashara yake yote kabla ya
kuifanya kwani mpango wa biashara hugusa kila kipengele kinachohusiana na
biashara kuanzia wasifu, umiliki, bidhaa/huduma, soko, utawala &
wafanyakazi, uendeshaji na fedha.
Kwahiyo ukijua kuandaa mpango wa biashara tayari ‘umehitimu
somo la biashara’ maana unakuwa hakuna kipengele kwenye biashara wewe
usichokijua. Ndio maana Self Help Books Tanzania chini ya blogu ya jifunzeujasiaramali
tukaanzisha mafunzo mahususi kwa ajili hiyo.
Tumefungua Darasa la kujifunza jinsi ya kuandaa
mpango/mchanganuo wa biashara yeyote ile bure. Mafunzo haya kupitia group la
watsap yanafanyika kila siku sambamba na masomo mengine ya fedha, biashara, ujasiriamali,
uchambuzi wa vitabu na ubunifu kwenye biashara.
Unapoingia tu darasani hivi unaanza masomo siku hiyohiyo
na unaweza kutumia kiungo kifuatacho kujiunga au kuwasiliana na sisi kwa namba
0765553030 tukuunganishe bure kabisa pamoja na kupatiwa vitabu mbalimbali bila
malipo
Karibu ujiunge hapa uanze kujifunza
leoleo
https://chat.whatsapp.com/CH2fntry2AbAB71sWhXh5B
Peter Tarimo
Mwalimu & Mtaalamu wa Michanganuo ya Biashara
Simu/watsap: 0765553030
0 Response to "NI NINI KULICHOKUWA NYUMA YA HARUSI HII NZURI YA KUPENDEZA?"
Post a Comment