CHAPATI BIASHARA YA MTAJI MDOGO INAYOHITAJI UJUZI MKUBWA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

CHAPATI BIASHARA YA MTAJI MDOGO INAYOHITAJI UJUZI MKUBWA

CHAPATI YA KAWAIDA YA KUSUKUMA
SUPU NA CHAPATI SEHEMU YA 1

Supu na chapati ni biashara ya mtaji mdogo unayoweza kuanzisha ukiwa hata na mtaji usiozidi laki 3, kina mama wengi huanza biashara ya kupika chapatiwakiwa hata na mtaji wa kununulia unga na mafuta tu, hitaji kubwa kwenye biashara hii ni mtu kuujua utaalamu wa kupika chapati laini na nzuri, supu tamu na iliyo na ladha ya kupendeza.

Katika somo letu hili la biashara ya Supu na Chapati tutakuwa na sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza itahusiana na chapatu tu, maandalizi yake na jinsi ya kuzipika halafu sehemu ya pili na ya mwisho itahusiana na Supu tu, maandalizi yake na jinsi ya kuitengeneza.

 

SEHEMU YA 1 CHAPATI

Ukiwa na ujuzi wa kutengeneza chapati laini na tamu unaweza ukapata fursa mbalimbali kama vile, tenda za kupika chapati kwenye shughuli mbalimbali, kazi katika hoteli na migahawa, kufungua biashara yako mwenyewe ya kupika supu na chapati na hata kukodiwa kupika chapati katika biashara za watu wengine ambao ujuzi huu hawana, kumbuka watu wengi hawana ujuzi huu. Lakini pia ukijua kupika chapati laini itakusaidia wewe mwenyewe kupika chapati nyumbani kwako na kufurahia na familia.

Asili ya chapati ni wapi?

Chapati (Roti) ni aina ya mkate bapa unaotengenezwa kwa unga wa ngano ambao asili yake ni huko nchini India na Pakistan.

Chakuala hiki kitamu kimekuwa kikipikwa huko kwa takriban miaka zaidi ya elfu 6 iliyopita na hatimaye zikaja kuenea katika maeneo mengine ya Dunia ikiwemo pia na Afrika ya Mashariki, Ulaya na Amerika nyakati watu walipoanza safari za kuvuka mabara katika harakati za kufanya biashara na uvumbuzi wa  nchi mpya.

SOMA: Biashara ndogondogo kwa wajasiriamali zinazoendana na wakatu tulio nao

Kwa sasa hivi chapati zinapendwa sana katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda na watu wengi hufanya biashara ya kupika na kuuza chapati.

Aina za Chapati

Kuna aina nyingi sana za chapatti hasa nchini India na Pakistan lakini kwa hapa kwetu Afrika Mashariki aina zilizozoeleka sana za chapati ni hizi zifuatazo;

1.  Chapati za kusukuma za kawaida

2.  Chapati mchambuko za kusukuma

3.  Chapati za maji

4.  Chapati za mayai na mbogamboga(Rolex)

1. Chapati za kusukuma za kawaida

Hizi ni chapatti rahisi kutengeneza na husukumwa mara moja tu bila ya kurudia mara mbili, ni laini ukifuata taratibu zinazostahili kutengeneza.

2. Chapati Mchambuko za kusukuma

Hizi zinafanana sana na zile za kawaida lakini tofauti yake kubwa ni kwamba zina matabaka yanayochambuka wakati wa kula(layers). Tabaka hizi hutokana na chapati kusukumwa mara ya pili baada ya mara ya kwanza kuviringishwa kama mkeka.

SOMA: Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado

3. Chapati za maji:

Chapati hizi hutengenezwa kwa uji mwembamba mbichi wa unga wa ngano uliokorogwa badala ya kusukuma kama ilivyo kwa aina nyinginezo hapo juu. Ni laini sana.

4. Rolex

Ni chapati za kawaida au mchambuko zilizoviringishwa ndani yake mayai na mbogamboga za majani, ni maarufu zaidi nchini Uganda

Watu wengi wanapendelea zaidi chapati za kusukuma iwe ni zile za kawaida ama zile mchambuko ilimradi tu ziwe laini na tamu lakini mtihani mkubwa katika uandaji wa chapati unabakia kuwa ni kwa namna gani chapati zinaweza kuwa laini na ladha ya kupendeza kila siku upikapo pasipo tena kubahatisha mara leo ni laini kesho ngumu, keshokutwa laini nk.

SOMA: Biashara ya Supu na Chapati

Somo letu hili tumelenga zaidi mbinu za kuhakikisha chapati zako zinakuwa laini na zenye ladha ya kupendeza kila mara pasipo kubahatisha, tutakupatia formula maalumu ya kutengeneza chapati.

SIRI ZA CHAPATI KUWA LAINI

Chapati kuwa ngumu ndiyo changamoto moja kubwa zaidi wapishi wa chapatti wanayokumbana nayo kote duniani. Kuna wakati chapatti zinaweza kukauka na kuvunjika utafikirizimeanikwa juani.

Wengine huamua kuongeza vitu mbalimbali kwenye chapati wakidhania ndi vitasaidia zisiwe ngumu lakini wala havisaidii, wanaongeza maziwa, asali, wengine mpaka hamira. Huhitaji kuongeza chochote zaidi ya vile vitu vya msingi tutakavyovitaja hapa labda tu sukari kidogo kwa ajili ya kuongeza ladha ya chapati.

Hapa nakushirikisha baadhi ya mbinu ambazo nilijifunza kwa tabu sana mwenyewe kutokana na uzoefu kwa muda mrefu wateja wakilalamika chapati zangu ni ngumu. Ni utaalamu mtu anaoweza kuupata tu kupitia uzoefu lakini mimi hapa nitakupatia kwa siku moja uwe kama umejifunza mwaka mzima.

MAANDALIZI:

VIFAA:

·       Beseni/Chombo cha kukandia unga

·       Kijiko cha kupimia chumvi na sukari

·       Kikombe cha kupimia maji

·       Jiko la mkaa/gesi kwa ajili ya kupikia chapati

·       Kikaangio/Chuma cha kupikia chapati(frying pan)

·       Mti wa kusukumia chapati/chupa ya soda

·       Kibao cha kusukumia chapati au meza

·       Kitambaa cha jikoni

·       Chombo cha kuweka chapati baada ya kuipua/hotpot

MAHITAJI / VIAMBATO / INGREDIENTS

1.  Unga wa ngano kilo 1

2.  Mafuta ya maji au samli vijiko 3 au 4

3.  Chumvi kijiko 1

4.  Maji vikombe 2

5.  Sukari kijiko 1

 

Maelezo nitakayoyatoa hapa kwenye blogu hii ni ya kawaida sawa tu na yale unayoweza kuyapata mahali kwingine kokote mtandaoni na nje ya mtandao lakini kuna sehemu kadhaa nimeruka siri ambazo ndiyo watu wengi wanapokwamia chapati zao zinakuwa ngumu. Kwenye maelezo yangu katika group la MICHANGANUO-ONLINE siri hizo zote nimeziweka bayana.

MAELEKEZO JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA KAWAIDA

1.  Changanya unga, chumvi na sukari kwenye beseni au chombo ulichoandaa, unaweza hapohapo ukaweka na mafuta au ukasubiri mpaka baadae kidogo ukishaanza kukanda. Kisha anza kuchanganya pamoja huku ukitia maji kidogokidogo mpaka mchanganyiko ugeuke kuwa donge. Endelea kukanda kwa dakika 10 – 15 mpaka donge liache kushikamana na chombo unachosukumia.

SOMA: Uzoefu wangu binafsi kwenye biashara ya supu na chapati laini za kusukuma

 

2.  Kata matonge madogomadogo saizi unayotaka chapati zako ziwe na uyapange ndani ya beseni kisha funika kwa kitambaa cha jikoni au taulo kwa dakika nyingine 10 – 15

 

3.  Tayarisha jiko lako likiwaka uweke kikaango juu yake kianze kuapata joto, moto uwe wa wastani lakini wa kutosha siyo mdogo sana.

 

4.  Anza kusukuma chapati zako ukianza na ile uliyoanza kuviringisha kwa kutumia mti wa kusukumia, tia juu ya kibao unga mkavu kidogo ili donge lisinase juu ya kibao

 

5.  Iweke chapati uliyosukuma juu ya kikaangio chako cha moto kwa sekund 10 – 15 kisha igeuze upande wa pili. Ikianza kubadilika rangi tia mafuta kidogo na kijiko huku ukiizungushazungusha, upande huo ukiiva igeuze upande mwingine nao ufanye hivyohivyo mpaka iive uitoe na kuiweka katika chombo au hotpot

 

6.  Rudia namba 5 mpaka umemaliza madonge yote uliyokata

 

7.  Sasa unaweza kula chapati zako au kuziuza kwa wateja.

Maelezo hayo hapo juu ndiyo maelezo unayoweza kuyapata sehemu nyingine karibu zote lakini bado kuna vitu vingi havipo wazi. Unaweza kuyafuata kweli chapati zako kwa bahati zikawa laini lakini pia zinaweza zisiwe laini kwa hiyo ni suala la kubahatisha.

Ukitaka maelekezo yenye siri zote za chapati kuwa laini, karibu ndani ya group letu la masomo ya kila siku, MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP

Kujiunga Lipia kiingilio chako sh. elfu 10 kwa namba zetu 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma ujumbe watsap au SMS usemao; 

"NIUNGE MASTERMIND GROUP NA OFFA YA VITU 22"

Tuma na anuani yako ya email kwa ajili ya kutumiwa offa ya vitu 22

0 Response to "CHAPATI BIASHARA YA MTAJI MDOGO INAYOHITAJI UJUZI MKUBWA"

Post a Comment