SUPU NA CHAPATI SEHEMU YA 1
Supu na chapati ni biashara ya mtaji mdogo unayoweza kuanzisha
ukiwa hata na mtaji usiozidi laki 3, kina mama wengi huanza biashara ya kupika
chapatiwakiwa hata na mtaji wa kununulia unga na mafuta tu, hitaji kubwa kwenye
biashara hii ni mtu kuujua utaalamu wa kupika chapati laini na nzuri, supu tamu
na iliyo na ladha ya kupendeza.
Katika somo letu hili la biashara ya Supu na Chapati
tutakuwa na sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza itahusiana na chapatu tu,
maandalizi yake na jinsi ya kuzipika halafu sehemu ya pili na ya mwisho
itahusiana na Supu tu, maandalizi yake na jinsi ya kuitengeneza.
SEHEMU
YA 1 CHAPATI
Ukiwa na ujuzi wa kutengeneza chapati laini na tamu
unaweza ukapata fursa mbalimbali kama vile, tenda za kupika chapati kwenye shughuli
mbalimbali, kazi katika hoteli na migahawa, kufungua biashara yako mwenyewe ya
kupika supu na chapati na hata kukodiwa kupika chapati katika biashara za watu
wengine ambao ujuzi huu hawana, kumbuka watu wengi hawana ujuzi huu. Lakini pia
ukijua kupika chapati laini itakusaidia wewe mwenyewe kupika chapati nyumbani
kwako na kufurahia na familia.
Asili
ya chapati ni wapi?
Chapati (Roti) ni aina ya mkate bapa unaotengenezwa kwa
unga wa ngano ambao asili yake ni huko nchini India na Pakistan.
Chakuala hiki kitamu kimekuwa kikipikwa huko kwa takriban
miaka zaidi ya elfu 6 iliyopita na hatimaye zikaja kuenea katika maeneo mengine
ya Dunia ikiwemo pia na Afrika ya Mashariki, Ulaya na Amerika nyakati watu
walipoanza safari za kuvuka mabara katika harakati za kufanya biashara na
uvumbuzi wa nchi mpya.
SOMA: Biashara ndogondogo kwa wajasiriamali zinazoendana na wakatu tulio nao
Kwa sasa hivi chapati zinapendwa sana katika nchi za
Tanzania, Kenya na Uganda na watu wengi hufanya biashara ya kupika na kuuza chapati.
Aina
za Chapati
Kuna aina nyingi sana za chapatti hasa nchini India na
Pakistan lakini kwa hapa kwetu Afrika Mashariki aina zilizozoeleka sana za
chapati ni hizi zifuatazo;
1. Chapati
za kusukuma za kawaida
2. Chapati
mchambuko za kusukuma
3. Chapati
za maji
4. Chapati
za mayai na mbogamboga(Rolex)
1. Chapati
za kusukuma za kawaida
Hizi ni chapatti rahisi kutengeneza na husukumwa mara
moja tu bila ya kurudia mara mbili, ni laini ukifuata taratibu zinazostahili
kutengeneza.
2.
Chapati Mchambuko za kusukuma
Hizi zinafanana sana na zile za kawaida lakini tofauti
yake kubwa ni kwamba zina matabaka yanayochambuka wakati wa kula(layers). Tabaka hizi hutokana na chapati
kusukumwa mara ya pili baada ya mara ya kwanza kuviringishwa kama mkeka.
SOMA: Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado
3. Chapati
za maji:
Chapati hizi hutengenezwa kwa uji mwembamba mbichi wa
unga wa ngano uliokorogwa badala ya kusukuma kama ilivyo kwa aina nyinginezo
hapo juu. Ni laini sana.
4.
Rolex
Ni chapati za kawaida au mchambuko zilizoviringishwa
ndani yake mayai na mbogamboga za majani, ni maarufu zaidi nchini Uganda
Watu wengi wanapendelea zaidi chapati za kusukuma iwe ni
zile za kawaida ama zile mchambuko ilimradi tu ziwe laini na tamu lakini mtihani
mkubwa katika uandaji wa chapati unabakia kuwa ni kwa namna gani chapati
zinaweza kuwa laini na ladha ya kupendeza kila siku upikapo pasipo tena
kubahatisha mara leo ni laini kesho ngumu, keshokutwa laini nk.
SOMA: Biashara ya Supu na Chapati
Somo letu hili tumelenga zaidi mbinu za kuhakikisha chapati
zako zinakuwa laini na zenye ladha ya kupendeza kila mara pasipo kubahatisha,
tutakupatia formula maalumu ya kutengeneza chapati.
SIRI
ZA CHAPATI KUWA LAINI
Chapati kuwa ngumu ndiyo changamoto moja kubwa zaidi
wapishi wa chapatti wanayokumbana nayo kote duniani. Kuna wakati chapatti
zinaweza kukauka na kuvunjika utafikirizimeanikwa juani.
Wengine huamua kuongeza vitu mbalimbali kwenye chapati
wakidhania ndi vitasaidia zisiwe ngumu lakini wala havisaidii, wanaongeza
maziwa, asali, wengine mpaka hamira. Huhitaji kuongeza chochote zaidi ya vile
vitu vya msingi tutakavyovitaja hapa labda tu sukari kidogo kwa ajili ya
kuongeza ladha ya chapati.
Hapa nakushirikisha baadhi ya mbinu ambazo nilijifunza
kwa tabu sana mwenyewe kutokana na uzoefu kwa muda mrefu wateja wakilalamika
chapati zangu ni ngumu. Ni utaalamu mtu anaoweza kuupata tu kupitia uzoefu
lakini mimi hapa nitakupatia kwa siku moja uwe kama umejifunza mwaka mzima.
MAANDALIZI:
VIFAA:
· Beseni/Chombo
cha kukandia unga
· Kijiko
cha kupimia chumvi na sukari
· Kikombe
cha kupimia maji
· Jiko
la mkaa/gesi kwa ajili ya kupikia chapati
· Kikaangio/Chuma
cha kupikia chapati(frying pan)
· Mti
wa kusukumia chapati/chupa ya soda
· Kibao
cha kusukumia chapati au meza
· Kitambaa
cha jikoni
· Chombo
cha kuweka chapati baada ya kuipua/hotpot
MAHITAJI
/ VIAMBATO / INGREDIENTS
1. Unga
wa ngano kilo 1
2. Mafuta
ya maji au samli vijiko 3 au 4
3. Chumvi
kijiko 1
4. Maji
vikombe 2
5. Sukari
kijiko 1
Maelezo
nitakayoyatoa hapa kwenye blogu hii ni ya kawaida sawa tu na yale unayoweza
kuyapata mahali kwingine kokote mtandaoni na nje ya mtandao lakini kuna sehemu
kadhaa nimeruka siri ambazo ndiyo watu wengi wanapokwamia chapati zao zinakuwa
ngumu. Kwenye maelezo yangu katika group la MICHANGANUO-ONLINE siri hizo zote
nimeziweka bayana.
MAELEKEZO
JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA KAWAIDA
1. Changanya
unga, chumvi na sukari kwenye beseni au chombo ulichoandaa, unaweza hapohapo
ukaweka na mafuta au ukasubiri mpaka baadae kidogo ukishaanza kukanda. Kisha
anza kuchanganya pamoja huku ukitia maji kidogokidogo mpaka mchanganyiko ugeuke
kuwa donge. Endelea kukanda kwa dakika 10 – 15 mpaka donge liache kushikamana
na chombo unachosukumia.
SOMA: Uzoefu wangu binafsi kwenye biashara ya supu na chapati laini za kusukuma
2. Kata
matonge madogomadogo saizi unayotaka chapati zako ziwe na uyapange ndani ya
beseni kisha funika kwa kitambaa cha jikoni au taulo kwa dakika nyingine 10 –
15
3. Tayarisha
jiko lako likiwaka uweke kikaango juu yake kianze kuapata joto, moto uwe wa
wastani lakini wa kutosha siyo mdogo sana.
4. Anza
kusukuma chapati zako ukianza na ile uliyoanza kuviringisha kwa kutumia mti wa
kusukumia, tia juu ya kibao unga mkavu kidogo ili donge lisinase juu ya kibao
5. Iweke
chapati uliyosukuma juu ya kikaangio chako cha moto kwa sekund 10 – 15 kisha
igeuze upande wa pili. Ikianza kubadilika rangi tia mafuta kidogo na kijiko
huku ukiizungushazungusha, upande huo ukiiva igeuze upande mwingine nao ufanye
hivyohivyo mpaka iive uitoe na kuiweka katika chombo au hotpot
6. Rudia
namba 5 mpaka umemaliza madonge yote uliyokata
7. Sasa
unaweza kula chapati zako au kuziuza kwa wateja.
Maelezo hayo hapo juu ndiyo maelezo unayoweza kuyapata
sehemu nyingine karibu zote lakini bado kuna vitu vingi havipo wazi. Unaweza
kuyafuata kweli chapati zako kwa bahati zikawa laini lakini pia zinaweza zisiwe
laini kwa hiyo ni suala la kubahatisha.
Ukitaka
maelekezo yenye siri zote za chapati kuwa laini, karibu ndani ya group letu la
masomo ya kila siku, MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP
Kujiunga Lipia kiingilio chako sh. elfu 10 kwa namba zetu 0712202244 au 0765553030 jina Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma ujumbe watsap au SMS usemao;
"NIUNGE MASTERMIND GROUP NA OFFA YA VITU 22"
Tuma na anuani yako ya email kwa ajili ya kutumiwa offa ya vitu 22
0 Response to "CHAPATI BIASHARA YA MTAJI MDOGO INAYOHITAJI UJUZI MKUBWA"
Post a Comment